Saturday, November 29, 2014

Kilichosemwa na Kamanda Kova na Waziri Lazaro Nyalandu kuhusu ajali ya Helikopta (Picha+Story)

Taarifa ambayo imeripotiwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ni kuhusu watu wanne kufariki kutokana na ajali ya Helikopta inayomilikiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, yenye namba 5HTWA kuanguka katika eneo la Kipunguni B, Ukonga Dar es salaam. Akizungumza na...
Read More »

Nigeria:Raia watakiwa kuwa waangalifu

Rais wa Nigeria Goodluck Johnathan amewataka raia kuwa waangalifu kufuatia shambulizi la bomu katika msikiti mmoja nchini humo
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amewataka watu wote nchini Nigeria kuwa waangalifu na kushirikiana na vikosi vya usalama vya nchi hiyo ili kujaribu kuzuia mashambulizi zaidi yanayotekelezwa na wanamgambo wa Boko Haram kaskazini mwa nchi.
   Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulizi hilo lililotokea kwenye msikiti mmoja mkubwa ulio kwenye mji wa Kano ambapo watu kadhaa waliuawa.
    Hata hivyo shambulizi hilo linaaminika kutekelezwa na Boko     Haram ambalo kampeni yake dhidi ya serikali imesababisha vifo vya maelfu ya watu mwaka huu.
   Polisi walitibua njama ya shambulizi jingine kwenye mji ulio kaskazini mwa Nigeria wa Maiduguri ambapo mabomu sita yaliharibiwa ndani ya msikiti mmoja na kwenye soko lililo karibu.

Tibaijuka:''Nilipokea pesa za Escrow''


Mjadala kuhusu kashfa ya uchotaji wa mamilioni ya fedha katika akaunti ya ESCROW ya Benki Kuu ya Tanzania umezidi kuunguruma nchini Tanzania kufuatia taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, PAC, na ripoti ya serikali kuhusu kashafa hiyo.
Mambo yaliyojitokeza katika ripoti ya PAC ni kutaja majina ya viongozi na maafisa wandamizi wa serikali walionufaika na magao huo.

Wednesday, November 26, 2014

habari iliyopo mtaani

Makamu Rais Zimbabwe atimuliwa ZANU-PF

Makamu wa Rais wa Zimbabwe Joyce Mujuru
Vyombo vya habari vya Serikali nchini Zimbabwe vinaripoti kuwa Makamu wa Rais,Joyce Mujuru, ameondolewa kwenye kamati kuu ya chama cha ZANU-PF.
Mujuru anashutumiwa kupanga mauaji dhidi ya Rais wa nchi hiyo,Robert Mugabe.
Hatua hiyo imekuja baada ya Kampeni dhidi ya Mujuru iliyofanywa na Mke wa Rais Mugabe, Grace ambaye kwa kiasi kikubwa anaamini anataka kumrithi Mumewe atakapotoka madarakani.
Viongozi kadhaa wa ZANU-PF wameshindwa kutetea nafasi zao katika Chama hicho.
Bi Mujuru alitarajiwa kumrithi rais Mugabe mwenye umri wa miaka tisini.
Kamati ya uchaguzi katika mkoa wa kaskazini wa Mashonaland ya kati imekataa wasifu wa Makamu wa rais nchi hiyo Joice Mujuru kama baadhi ya stakabadhi zake za kuomba kazi katika uchaguzi uliofanyika siku ya Jumanne.


  


Tuesday, November 25, 2014

Zaidi ya watu 60 wauawa Syria

 Majeshi ya Syria yafanya mashambulizi

Zaidi ya watu 60 wameuwawa, katika mashambulio kadhaa ya angani yaliyofanywa na Jeshi la serikali ya Syria.
Raia wengi waliuwawa katika mashambulio tisa yaliyolenga ngome kuu za kundi la wapiganaji wa Islamic State.
Wakereketwa wameiambia BBC kuwa Hospitali kuu ya Raqqa imesalia bila huduma kwani HAKUNA chakula na umeme.

Miili yatelekezwa Sierra Leone

  Wafanyakazi ambao huzika miili ya Watu waliokufa kwa Ebola, mjini Kenema nchini Sierra Leone wamegoma kwa sababu hawajalipwa marupurupu yao.
Miili 15,kati ya hiyo mingi inahitajika kuzikwa,imetelekezwa katika hospitali kuu mjini humo.
Mwili mmoja unadaiwa kutelekezwa kwenye Ofisi ya Meneja wa Hospitali hiyo, huku miili miwili ikiwa imetelekezwa kwenye mlango wa kuingilia Hospitali hapo.

Wafanyakazi hao wameiambia BBC kuwa hawajalipwa marupurupu ya waliyoyaita ya hatari kama walivyoahidiwa kwa ajili ya Mwezi Oktoba na Novemba.
Kenema ni mji wa tatu kwa ukubwa nchini Sierra Leone na Mkubwa katika eneo la Mashariki mwa nchi hiyo ambako ugonjwa huo uligunduliwa kwa mara ya kwanza.
Takriban Watu 5000 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huu katika nchi za Magharibi mwa Afrika, Guinea,Liberia na Sierra Leone.

P-Square wamepata pigo lingine,wamefiwa na baba yao mzazi.

Mapacha kutoka nchini Nigeria Peter Okoye&Paul Okoye P- Square pamoja na kaka yao Jude Okoye,Jumatatu ya Nov 24 wamempoteza mzazi aliyebakia ambaye ni baba yao mzazi hii ni miaka miwili tangu afariki mama yao.






tovuyi ya www.Naij.com imesema kuwa Mr.Okoye alikua akisumbuliwa na maumivu ya Goti baada ya kufanyiwa upasuaji ingawa hali iliripotiwa kuendelea vizuri.



Monday, November 24, 2014

Mabibi na mabwana… ile single mpya ya Ay ft. Sean Kingston imetoka, isikilize hapa


Ay 1Ay ametimiza ahadi yake ya kuiachia ile kolabo yake na Sean Kingston ambayo hivi karibuni ndio ilimpeleka Marekani kwenda kufanya video na mkali huyu wa dunia.
Jisikie huru kubonyeza hapa ili kuisikiliza hii new single >>> HAPA

Bunduki bandia yamletea maafa US


Kijana Tamir Rice alipigwa risasi mbili baada ya kupatikana na kilichibainika kuwa budnuki bandia
    
     Wakili anayewakilisha familia ya kijana mweusi mwenye umri wa miaka kumi na mbili aliyepigwa risasi na polisi katika mji wa Cleveland nchini Marekani, amesema familia yake itafanya uchunguzi wake sambamba na ule unaofanywa na Polisi kubaini kilichotokea.
        Kijana huyo kwa jina Tamir Rice mwenye umri wa miaka 12 alikuwa amebeba kile kilichoonekana kuwa bunduki bandia. Polisi wanadai kuwa kijana huyo alikataa kutii amri alipoambaiwa asalimu amri.
             Kifaa walichokuwa nacho polisi ndicho kilibaini kuwa bunduki hiyo ilikuwa bandia.
Inaarifiwa kijana huyo alipigwa risasi mara mbili baada ya kuitoa bunduki yake kiunoni mwake lakini hakujaribu hata wakati mmoja kuielekeza kwa poliso wala kujribu kuifyatua.
      Wakili wa familia hiyo amesema kuwa ikiwa watapata kuwa haki za kijana huyo zilikiukwa, familia yake itachukua hatua za kisheria dhidi ya polisi.
           Mwanasiasa mmoja anapendekeza sheria ambayo itahakikisha kuwa bunduki bandia zinakuwa na rangi unayong'aa zaidi ili ziweze kutambulika haraka.

Mama ashtakiwa kutupa mtoto Sydey


 Mtoto anayekisiwa kuwa na umri wa wiki moja aliokotwa na waendesha baiskeli
   Mama mmoja nchini Australia anashtakiwa kwa kosa la jaribio la mauaji dhidi ya mtoto wake mchanga ambaye alikutwa akilia katika eneo alilotelekezwa kwenye mfereji unaopitisha maji machafu pembeni ya barabara mjini Sydney,ambapo Polisi wanakisia kuwa mtoto huyo alikuwa katika eneo hilo kwa siku tano.
   Waendesha baiskeli walisikia sauti ya mtoto ikitokea kwenye eneo hilo siku ya jumapili.
    Mwanamke huyo,Saifale Nai alitiwa nguvuni na Polisi baada ya msako uliodumu kwa saa kadhaa kwa kupata taarifa katika hospitali na operesheni ya nyumba kwa nyumba.
Polisi inasema mtoto huyo wa kiume alitupwa tangu siku ya jumanne .

  Taarifa za mahakama zinasema mwanamke huyo alikubali kuwa alimtupa mtoto wake katika mfereji huo akiamini kuwa angekufa.
  Mtoto huyo anaelezwa kuwa yuko hospitalini na hali yake inaendelea vizuri