Nigeria:Raia watakiwa kuwa waangalifu
Rais wa Nigeria Goodluck Johnathan amewataka raia kuwa waangalifu kufuatia shambulizi la bomu katika msikiti mmoja nchini humo
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan
amewataka watu wote nchini Nigeria kuwa waangalifu na kushirikiana na
vikosi vya usalama vya nchi hiyo ili kujaribu kuzuia mashambulizi zaidi
yanayotekelezwa na wanamgambo wa Boko Haram kaskazini mwa nchi.
Hakuna
kundi lililodai kuhusika na shambulizi hilo lililotokea kwenye msikiti
mmoja mkubwa ulio kwenye mji wa Kano ambapo watu kadhaa waliuawa.Hata hivyo shambulizi hilo linaaminika kutekelezwa na Boko Haram ambalo kampeni yake dhidi ya serikali imesababisha vifo vya maelfu ya watu mwaka huu.
Polisi walitibua njama ya shambulizi jingine kwenye mji ulio kaskazini mwa Nigeria wa Maiduguri ambapo mabomu sita yaliharibiwa ndani ya msikiti mmoja na kwenye soko lililo karibu.
Tibaijuka:''Nilipokea pesa za Escrow''
Mjadala kuhusu kashfa ya uchotaji wa mamilioni ya fedha katika akaunti ya ESCROW ya Benki Kuu ya Tanzania umezidi kuunguruma nchini Tanzania kufuatia taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, PAC, na ripoti ya serikali kuhusu kashafa hiyo.Mambo yaliyojitokeza katika ripoti ya PAC ni kutaja majina ya viongozi na maafisa wandamizi wa serikali walionufaika na magao huo.
No comments:
Post a Comment