Baada ya Taarifa rasmi kutoka klabu ya Yanga December 15, 2014 kuwa
kocha Mbrazil Marcio Maximo ameondoka ndani ya timu hiyo baada ya
uongozi wa Yanga kufikia makubaliano naye ya kuvunja
mkataba, Marcio Maximo aondoka rasmi nchini kurejea kwao nchini Brazil
na ndege ya shirika la ndege la Emirates.