Tuesday, March 10, 2015

AKUTWA AMEUAWA NA KUNYOFOLEWA SEHEMU ZA SIRI




MTU MMOJA MKAZI WA UTURO WILAYANI MBARALI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA CHARLES SIJAONA @ MATEMLA (55) ALIKUTWA AMEUAWA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA KWA KUKATWA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA KICHWANI NA SHINGONI. AIDHA MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA UKIWA UMENYOFOLEWA SEHEMU ZA SIRI NA WATU HAO.
MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA NJE YA NYUMBA ALIYOKUWA AKIISHI MNAMO TAREHE 08.03.2015 MAJIRA YA SAA 01:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA UTURO, KATA YA MAPOGOLO, TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA.
CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO HAKIJAFAHAMIKA, JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILO ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI NYIGESA R. WANKYO ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO. AIDHA MSAKO/UPELELEZI WA KUWABAINI WALIHUSIKA KATIKA TUKIO HILI UNAENDELEA.

Ushirikina kamwe hauwezi kuinua soka Bongo

Shabiki wa Yanga akishangilia kwa mtindo wa kuvaa hirizi na kushika njiwa, vitu ambavyo hutumika sana na waganga wa kienyeji. 


Posted  Jumatatu,Marchi9  2015  saa 12:7 PM
In Summary
Moja ya ndoto hizo ni kuhakikisha Tanzania inafuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) kwani tangu Taifa Stars ifuzu mwaka 1980 hadi sasa haijafuzu tena.



KAMA zilivyo nchi nyingine za Afrika, soka la Tanzania bado lipo chini, ni nchi ambayo inajikongoja kukamilisha ndoto zake.
Moja ya ndoto hizo ni kuhakikisha Tanzania inafuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) kwani tangu Taifa Stars ifuzu mwaka 1980 hadi sasa haijafuzu tena.
Kumekuwa na juhudi mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanyika ili kuikomboa Tanzania na kuhakikisha inafuzu kushiriki fainali hizo.
Ni hivi karibuni tu tumeshuhudia harakati za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kushirikiana na klabu ya Barcelona kuanzisha chuo cha soka kwa vijana wa umri mdogo mjini Kigamboni.
Mbali na taasisi hiyo, watu binafsi nao wamekuwa mstari wa mbele katika kuanzisha shule za soka lengo likiwa ni hilo hilo la kutengeneza vipaji vya soka ambavyo vitakuwa na maana kwa taifa.
Hata hivyo katika hali ya kushangaza wakati baadhi ya watu wakiamini kuwekeza kwenye soka la vijana wadogo, wengine wanawekeza katika mbinu nyingine ambazo kimsingi zimepitwa na wakati.
Mbinu hizo ni kuwa na imani za ushirikina ambao wapo baadhi ya watu katika klabu wanaoamini bila kujihusisha na ushirikina hawataweza kupata matokeo mazuri katika timu zao.
Inasikitisha kuona kwamba wapo watu ambao hudiriki kutumia fedha nyingi kwa ajili ya mambo ya ushirikina na kutaka kutengewa bajeti maalum ya mambo hayo.
Hili kwetu bado tunaliona kuwa ni tatizo kubwa ambalo kama halitafanyiwa kazi basi mipango yote ya maendeleo ya soka itaendelea kukwama.
Ni tatizo kubwa hasa inapobainika kwamba klabu kubwa na kongwe za Simba na Yanga ndizo zinazoongoza katika mambo haya ya ushirikina.
Kabla ya mechi ya ya jana, Jumapili, klabu hizo zilihama jijini Dar es Salaam, Simba waliweka kambi Zanzibar wakati Yanga wao wakaweka kambi Bagamoyo.
Hatuna tatizo na uamuzi wa klabu hizi kutoka nje ya jiji la Dar es Salaam kutokana na umuhimu wa mechi yao lakini inasikitisha pale unaposikia kwamba sababu ya kwenda huko ni kurahisisha mambo ya ushirikina.