Friday, January 23, 2015

Ligi kuu Tanzania kuendelea Jumamosi



 
Ligi kuu ya Tanzania itaendelea Jumamosi hii huku mechi kadhaa zikichezwa ikiwemo ile kati ya bingwa mtetezi na wawakilishi wa nchi katika michuano ya klabu bingwa Afrika, Azam FC na Simba Sports Club ikiwa chini ya kocha Mserbia, Goran Kopunovic.
Azam inaongoza ligi ikiwa na pointi 20 na baada ya mechi yao na Simba itaenda Jamhuri ya Kongo (DRC) kwa ajili ya kucheza mechi za majaribio kwa ajili ya mechi yao na vigogo wa Sudan, El-Merreikh katika mechi ya kwanza klabu bingwa Afrika itakayochezwa Dar es Salaam kati kati ya mwezi ujao.
Mabingwa wa zamani wa Tanzania na wawakilishi wa nchi katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika, Yanga, ikiwa ya nne katika msimamo na alama (points) 15, watacheza na Polisi Morogoro wakati Mtibwa Sugar, ikiwa ya pili na alama 17, watacheza na Ruvu Shooting.
Mechi nyingine ni kama ifuatavyo
Stand United vs Coastal Union-Uwanja wa Kambarage,Shinyanga
Kagera Sugar vs Ndanda-Uwanja wa Kaitaba, Kagera
Mbeya City vs Tanzania Prisons-Uwanja wa Sokoine, Mbeya

Ishu ya Wema Sepetu kuhusu kumdai Diamond, majibu ya Wema ni haya hapa


sptUkubwa wa story hii ambayo jana aliizungumzia Martin Kadinda, Meneja wa Wema Sepetu imefanya millardayo.com kumtafuta Wema ili kuujua undani zaidi juu ya ishu hii ambayo ilichukua headlines kubwa Magazetini na mitandaoni pia.
Kwenye Exclusive Interview, Wema Sepetu amesema haya;
Taarifa hii imenishtua sana maana asubuhi ya jana nimekuta kwenye gazeti wameandika nikashangaa yaani hapa nimekaa kwa sababu muda mwingi siendeshi mimi akaunti yangu ya twitter, anaiendesha mtu wangu wa blog Bestizo maana nilikua nataka kutoa tamko-- Wema Sepetu.
Nilishasema ukurasa huu tulishaufunga na nilishasema haiwezi kujirudia tena, nashangaa watu wanarudi na maneno yale yale maana nimekaa kimya kwa kila kitu ili kuepuka haya maneno
Hakuna kitu ambacho namdai Diamond,hakuna siku hata moja nimefikiria kwenda kumshtaki Diamond labda kama kungekua kuna kitu chochote,yaani labda kungekua na ukweli wa kitu chochote siwezi kupoteza muda wangu kwenda polisi,sijawahi kufanya kitu cha namna hii hizi taarifa zimenishtua sana
Sijawahi kujiunga VICOBA maana sivijui, nilikua nimekaa na mtu akanambia labda Wema hujui  hawa watu wa VICOBA wanajaribu kujitangaza kwa njia hii na kutengeneza hii kitu kwamba VICOBA wanaweza kukopa hadi Milioni kumi… kwanza mimi siwezi kukopa Milioni 10“– Wema Sepetu.

Wednesday, January 21, 2015

Daladala ziligoma leo Arusha, ni Bodaboda tu barabarani…


BODAWaendesha bodaboda wa Arusha leo wamejikuta kwenye jukumu la daladala kusafirisha abiria baada ya mgomo wa daladala uliofanywa leo maeneo ya mji huo sababu ikitajwa ni kuanzishwa kwa route mpya wanayotakiwa kuanza hivi sasa kutoka Njiro na Moshono kuelekea mjini.
Wakazi wengi wa mji huo leo wamelazimika kutembea kwa miguu huku wengine wenye uwezo wakitumia usafiri wa bodaboda.
Bodaboda
Ripota wa Blog ya Michuzi ambaye ameripoti kuhusu story hii amesema yeye pia alikuwa mmoja ya walioathirika kutokana na mgomo huo

Sunday, January 18, 2015

HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA YATOA UFAFANUZI WA SINTOFAHAMU UKARABATI WA BARABARA YA IGANZO- KABWE.

Mhandisi wa Jiji la Mbeya, Laynas Sanya, akizungumza na vyombo vya habari Iganzo jijini Mbeya kuhusiana na ukarabati wa barabara ya Iganzo- Kabwe.

Mhandisi Msaidizi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Injinia Chaula, ambaye ndiye anayesimamia barabara hiyo akionesha namna Greda linavyopasa kusembua kifusi kabla ya kushindilia.

Afisa Mstaafu wa Idara ya ujenzi mkoani Mbeya,Betwel Mbelile akionesha kushangazwa na namna barabara hiyo inavyokarabatiwa.


Sehemu ya barabara ambayo imekamilika baada ya kumwagwa kifusi na kushindiliwa tayari kwa kuanza kutumika.


UONGOZI wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya umelazimika kutoa ufafanuzi wa sintofahamu kuhusu ukarabati wa barabara ya Iganzo- Kabwe kufuatia malalamiko ya baadhi ya wananchi.


Baadhi ya Wakazi wa Isanga walitoa malalamiko yako kwa vyombo vya habari wakilalamikia hatua zilizocghukuliwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa kuamua kukarabatio Barabara ya Iganzo- Kabwe kwa kufukia vifusi vya mawe juu ya Lami huku wakihofia mvua zinazonyesha kuweza kuharibu.


Kutokana na malalamiko hayo na kuripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari baada ya uongozi wa Jiji kushindwa kujitokeza ili kuyatolea ufafanuzi ndipo Mhandisi wa Jiji la Mbeya, Laynas Sanya, akalazimika kufika eneo la mradi na kuzungumza na vyombo vya habari.


Mhandisi Sanya alisema ukarabati unaofanyika katika barabara hiyo ni kwa ajili ya kupitika katika kipindi kifupi wakati Uongozi wa Jiji ukijipanga kufanya ukarabati mkubwa hivyo kulazimika kuziba kwenye sehemu zilizokuwa zimechimbika sana huku sehemu nzuri zikirukwa.


Alisema baada ya kifusi kumwagwa Greda hupita na kuvuruga sehemu ya Lami ilichini ikichanganya na kifusi kisha kushindiliwa vizuri hali itakayosaidia njia hiyo kupitika kirahisi na kurahisisha masuala ya usafiri kwa wakazi wa Jiji la Mbeya.


Aliongeza kuwa mbali na Halmashauri ya Jiji la Mbeya kukosa fedha za kujenga upya barabara hiyo pia ikio kwenye mazungumzo ya kuifanya Barabara hiyo kupandishwa hadhi na kuwa ya Mkoa.


Akizungumzia kuhusu vifaa na Ukandarasi alisema kazi hiyo inafanywa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa kufuata kanuni za manunuzi ya umma isipokuwa Vifaa vilikosekana na kulazimu kukodi kwa Mkandarasi wa kampuni ya China Communications Contractor Company Ltd(CCCC) na kufanya jumla ya gharama zote kufikia shilingi Milioni 37.


Mwisho.