Wednesday, November 26, 2014

habari iliyopo mtaani

Makamu Rais Zimbabwe atimuliwa ZANU-PF

Makamu wa Rais wa Zimbabwe Joyce Mujuru
Vyombo vya habari vya Serikali nchini Zimbabwe vinaripoti kuwa Makamu wa Rais,Joyce Mujuru, ameondolewa kwenye kamati kuu ya chama cha ZANU-PF.
Mujuru anashutumiwa kupanga mauaji dhidi ya Rais wa nchi hiyo,Robert Mugabe.
Hatua hiyo imekuja baada ya Kampeni dhidi ya Mujuru iliyofanywa na Mke wa Rais Mugabe, Grace ambaye kwa kiasi kikubwa anaamini anataka kumrithi Mumewe atakapotoka madarakani.
Viongozi kadhaa wa ZANU-PF wameshindwa kutetea nafasi zao katika Chama hicho.
Bi Mujuru alitarajiwa kumrithi rais Mugabe mwenye umri wa miaka tisini.
Kamati ya uchaguzi katika mkoa wa kaskazini wa Mashonaland ya kati imekataa wasifu wa Makamu wa rais nchi hiyo Joice Mujuru kama baadhi ya stakabadhi zake za kuomba kazi katika uchaguzi uliofanyika siku ya Jumanne.


  


Tuesday, November 25, 2014

Zaidi ya watu 60 wauawa Syria

 Majeshi ya Syria yafanya mashambulizi

Zaidi ya watu 60 wameuwawa, katika mashambulio kadhaa ya angani yaliyofanywa na Jeshi la serikali ya Syria.
Raia wengi waliuwawa katika mashambulio tisa yaliyolenga ngome kuu za kundi la wapiganaji wa Islamic State.
Wakereketwa wameiambia BBC kuwa Hospitali kuu ya Raqqa imesalia bila huduma kwani HAKUNA chakula na umeme.

Miili yatelekezwa Sierra Leone

  Wafanyakazi ambao huzika miili ya Watu waliokufa kwa Ebola, mjini Kenema nchini Sierra Leone wamegoma kwa sababu hawajalipwa marupurupu yao.
Miili 15,kati ya hiyo mingi inahitajika kuzikwa,imetelekezwa katika hospitali kuu mjini humo.
Mwili mmoja unadaiwa kutelekezwa kwenye Ofisi ya Meneja wa Hospitali hiyo, huku miili miwili ikiwa imetelekezwa kwenye mlango wa kuingilia Hospitali hapo.

Wafanyakazi hao wameiambia BBC kuwa hawajalipwa marupurupu ya waliyoyaita ya hatari kama walivyoahidiwa kwa ajili ya Mwezi Oktoba na Novemba.
Kenema ni mji wa tatu kwa ukubwa nchini Sierra Leone na Mkubwa katika eneo la Mashariki mwa nchi hiyo ambako ugonjwa huo uligunduliwa kwa mara ya kwanza.
Takriban Watu 5000 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huu katika nchi za Magharibi mwa Afrika, Guinea,Liberia na Sierra Leone.

P-Square wamepata pigo lingine,wamefiwa na baba yao mzazi.

Mapacha kutoka nchini Nigeria Peter Okoye&Paul Okoye P- Square pamoja na kaka yao Jude Okoye,Jumatatu ya Nov 24 wamempoteza mzazi aliyebakia ambaye ni baba yao mzazi hii ni miaka miwili tangu afariki mama yao.






tovuyi ya www.Naij.com imesema kuwa Mr.Okoye alikua akisumbuliwa na maumivu ya Goti baada ya kufanyiwa upasuaji ingawa hali iliripotiwa kuendelea vizuri.



No comments:

Post a Comment