
Shabiki wa Yanga akishangilia kwa mtindo wa kuvaa hirizi na kushika njiwa, vitu ambavyo hutumika sana na waganga wa kienyeji.
Posted Jumatatu,Marchi9 2015 saa 12:7 PM
In Summary
Moja ya ndoto hizo ni kuhakikisha Tanzania inafuzu
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) kwani tangu Taifa Stars
ifuzu mwaka 1980 hadi sasa haijafuzu tena.
KAMA zilivyo nchi nyingine za Afrika, soka la Tanzania bado lipo chini, ni nchi ambayo inajikongoja kukamilisha ndoto zake.
Moja ya ndoto hizo ni kuhakikisha Tanzania inafuzu
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) kwani tangu Taifa Stars
ifuzu mwaka 1980 hadi sasa haijafuzu tena.
Kumekuwa na juhudi mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanyika ili kuikomboa Tanzania na kuhakikisha inafuzu kushiriki fainali hizo.
Ni hivi karibuni tu tumeshuhudia harakati za
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kushirikiana na klabu ya
Barcelona kuanzisha chuo cha soka kwa vijana wa umri mdogo mjini
Kigamboni.
Mbali na taasisi hiyo, watu binafsi nao wamekuwa
mstari wa mbele katika kuanzisha shule za soka lengo likiwa ni hilo hilo
la kutengeneza vipaji vya soka ambavyo vitakuwa na maana kwa taifa.
Hata hivyo katika hali ya kushangaza wakati baadhi
ya watu wakiamini kuwekeza kwenye soka la vijana wadogo, wengine
wanawekeza katika mbinu nyingine ambazo kimsingi zimepitwa na wakati.
Mbinu hizo ni kuwa na imani za ushirikina ambao
wapo baadhi ya watu katika klabu wanaoamini bila kujihusisha na
ushirikina hawataweza kupata matokeo mazuri katika timu zao.
Inasikitisha kuona kwamba wapo watu ambao hudiriki
kutumia fedha nyingi kwa ajili ya mambo ya ushirikina na kutaka
kutengewa bajeti maalum ya mambo hayo.
Hili kwetu bado tunaliona kuwa ni tatizo kubwa
ambalo kama halitafanyiwa kazi basi mipango yote ya maendeleo ya soka
itaendelea kukwama.
Ni tatizo kubwa hasa inapobainika kwamba klabu
kubwa na kongwe za Simba na Yanga ndizo zinazoongoza katika mambo haya
ya ushirikina.
Kabla ya mechi ya ya jana, Jumapili, klabu hizo
zilihama jijini Dar es Salaam, Simba waliweka kambi Zanzibar wakati
Yanga wao wakaweka kambi Bagamoyo.
Hatuna tatizo na uamuzi wa klabu hizi kutoka nje
ya jiji la Dar es Salaam kutokana na umuhimu wa mechi yao lakini
inasikitisha pale unaposikia kwamba sababu ya kwenda huko ni kurahisisha
mambo ya ushirikina.
No comments:
Post a Comment