
Polisi nchini Kenya wanasema kuwa
wanamgambo wanaoshukiwa kuwa wa kundi la Al Shabaab wamewauwa kwa
kuwapiga risasi zaidi ya watu 28 waliokuwa wakisafiri kwenye basi moja
karibu na mpaka wa Somalia.
Maafisa wa ngazi ya juu wamesema kuwa
basi hilo lilitekwanyara katika Jimbo la Mandera wakati likiwa njiani
kuelekea katika mji mkuu Nairobi.
Watu wasiokuwa waislamu wanasemakana kutengwa na abiria wengine na kisha kupigwa risasi.
Kundi la al-Shabab nchini Somalia limetekeleza mashambulizi kadhaa nchini Kenya tangu mwaka 2011.
Huo ndio mwaka ambapo Kenya iliwatuma wanajeshi wake nchini Somalia kupigana na kundi hilo la waislamu wenye itikadi kali.
Mji
wa Mandera katika eneo la Kaskazini mashariki ndio ulioathirika
pakubwa. Baada ya shambulio hilo la mapema jumamosi maafisa katika eneo
hilo wamenukuliwa na vyombo vya habari nchini kenya wakisema kuwa
serikali ilikataa kuitikia ombi lao la kutaka usalama kudumishwa zaidi.
Afisa
mmoja ameliambia gazeti la Daily Nation kwamba wavamizi hao waliwataka
abiria kusoma aya katika Koran kabla ya kuwaangamiza walioshindwa
kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment