Tuesday, March 10, 2015

AKUTWA AMEUAWA NA KUNYOFOLEWA SEHEMU ZA SIRI




MTU MMOJA MKAZI WA UTURO WILAYANI MBARALI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA CHARLES SIJAONA @ MATEMLA (55) ALIKUTWA AMEUAWA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA KWA KUKATWA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA KICHWANI NA SHINGONI. AIDHA MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA UKIWA UMENYOFOLEWA SEHEMU ZA SIRI NA WATU HAO.
MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA NJE YA NYUMBA ALIYOKUWA AKIISHI MNAMO TAREHE 08.03.2015 MAJIRA YA SAA 01:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA UTURO, KATA YA MAPOGOLO, TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA.
CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO HAKIJAFAHAMIKA, JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILO ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI NYIGESA R. WANKYO ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO. AIDHA MSAKO/UPELELEZI WA KUWABAINI WALIHUSIKA KATIKA TUKIO HILI UNAENDELEA.

Ushirikina kamwe hauwezi kuinua soka Bongo

Shabiki wa Yanga akishangilia kwa mtindo wa kuvaa hirizi na kushika njiwa, vitu ambavyo hutumika sana na waganga wa kienyeji. 


Posted  Jumatatu,Marchi9  2015  saa 12:7 PM
In Summary
Moja ya ndoto hizo ni kuhakikisha Tanzania inafuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) kwani tangu Taifa Stars ifuzu mwaka 1980 hadi sasa haijafuzu tena.



KAMA zilivyo nchi nyingine za Afrika, soka la Tanzania bado lipo chini, ni nchi ambayo inajikongoja kukamilisha ndoto zake.
Moja ya ndoto hizo ni kuhakikisha Tanzania inafuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) kwani tangu Taifa Stars ifuzu mwaka 1980 hadi sasa haijafuzu tena.
Kumekuwa na juhudi mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanyika ili kuikomboa Tanzania na kuhakikisha inafuzu kushiriki fainali hizo.
Ni hivi karibuni tu tumeshuhudia harakati za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kushirikiana na klabu ya Barcelona kuanzisha chuo cha soka kwa vijana wa umri mdogo mjini Kigamboni.
Mbali na taasisi hiyo, watu binafsi nao wamekuwa mstari wa mbele katika kuanzisha shule za soka lengo likiwa ni hilo hilo la kutengeneza vipaji vya soka ambavyo vitakuwa na maana kwa taifa.
Hata hivyo katika hali ya kushangaza wakati baadhi ya watu wakiamini kuwekeza kwenye soka la vijana wadogo, wengine wanawekeza katika mbinu nyingine ambazo kimsingi zimepitwa na wakati.
Mbinu hizo ni kuwa na imani za ushirikina ambao wapo baadhi ya watu katika klabu wanaoamini bila kujihusisha na ushirikina hawataweza kupata matokeo mazuri katika timu zao.
Inasikitisha kuona kwamba wapo watu ambao hudiriki kutumia fedha nyingi kwa ajili ya mambo ya ushirikina na kutaka kutengewa bajeti maalum ya mambo hayo.
Hili kwetu bado tunaliona kuwa ni tatizo kubwa ambalo kama halitafanyiwa kazi basi mipango yote ya maendeleo ya soka itaendelea kukwama.
Ni tatizo kubwa hasa inapobainika kwamba klabu kubwa na kongwe za Simba na Yanga ndizo zinazoongoza katika mambo haya ya ushirikina.
Kabla ya mechi ya ya jana, Jumapili, klabu hizo zilihama jijini Dar es Salaam, Simba waliweka kambi Zanzibar wakati Yanga wao wakaweka kambi Bagamoyo.
Hatuna tatizo na uamuzi wa klabu hizi kutoka nje ya jiji la Dar es Salaam kutokana na umuhimu wa mechi yao lakini inasikitisha pale unaposikia kwamba sababu ya kwenda huko ni kurahisisha mambo ya ushirikina.

Wednesday, February 25, 2015

JESHI LA KUJENGA TAIFA TAARIFA KUHUSU VIJANA WALIOHITIMU MAFUNZO YA JKT KWA KUJITOLEA NA KUDAI KUAJIRIWA NA SERIKALI




Jeshi la Kujenga Taifa lilianzishwa Julai 10, 1963 na serikali kwa lengo la kuwaweka pamoja vijana wa nchi hii na kuwapa malezi kuhusu uzalendo na umoja ili kuondoa dalili za matabaka zilizoanza kujitokeza katika jamii baada ya uhuru.

                Baadhi ya sababu za kuanzishwa kwa JKT ni:
         Kubadili fikra za vijana wa nchi hii kutoka ile hali ya ukoloni kutegemea nchi nyingine kuleta maendeleo.

·           Kukusanya nguvu za vijana wote wa nchi hii na kuzielekeza kwa umoja wao kufanya kazi pamoja kwa manufaa ya taifa.

         Kuwafunza vijana kujenga mshikamano na umoja wa kitaifa, ili kulinda uhuru wa Taifa lao.

Jeshi la Kujenga Taifa linaunganisha vijana bila kujali itikadi zao, dini, elimu, jinsia na mali ili kuwalea kuwa wazalendo kwa taifa lao na kupenda kuitumikia nchi yao.

Pamoja na dhana ya kufunzwa uzalendo, pia stadi mbalimbali za kazi hufundishwa kwa vijana hao ili waweze kujiajiri, pindi wamalizapo mkataba yao ya kujitolea kwa miaka miwili.

Serikali ilirejesha mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa vijana wa kujitolea mwaka 2001, baada ya kusitishwa mwaka 1994.

Masharti ya Kujiunga na JKT kwa vijana wa Kujitolea
Kijana kabla ya kujiunga na JKT hutakiwa kuyajua masharti na kuzifahamu taratibu za kujiunga  na kuelewa kuwa JKT halitoi ajira.

Moja ya kipengele cha masharti ya kujiunga na JKT kinasema kuwa ‘Kwa kipindi chote nitakachokua ndani ya Jeshi la Kujenga Taifa nitakuwa nafanya mafunzo ya kijeshi na ya stadi za kazi na maisha, na baada ya mkataba nitarejea nyumbani. Hivyo sitalidai Jeshi la Kujenga Taifa ajira, wala kulitaka linitafutie ajira/kazi’.

Kipengele hiki kinaainisha masharti ya makubaliano kati ya Jeshi la Kujenga Taifa na kijana kabla ya kujiunga na kupatiwa mafunzo ya awali ya kijeshi.

Aidha, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wengine mara kadhaa wamekuwa wakisisitiza kuwa, JKT halitoi ajira.

Lakini hivi karibuni wakati nchi inaelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge mwaka huu, umezuka mtindo wa makundi ya vijana waliopitia JKT katika Operesheni mbalimbali kuomba kuandamana kwenda Ikulu kudai ajira.

Madai yanayopingana na dhana ya JKT na kauli ya Mhe. Rais kuwa Jeshi la Kujenga Taifa haliajiri, bali vijana hujiunga kwa hiari kwa kujitolea na baada ya mkataba wa miaka miwili wanatakiwa kurejea walikotoka.

Aidha, Mhe. Rais Kikwete, amewahi kutoa agizo kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, taasisi za Serikali na kuziomba zile zisizo za kiserikali kutoa ajira kwa vijana waliopata mafunzo ya JKT kulingana na sifa za kijana na nafasi zilizopo.

Takwimu zinaonesha kuwa tangu kurejeshwa kwa mafunzo ya JKT mwaka 2001 hadi mwaka jana, jumla ya vijana 104,594 wamejiunga na JKT wakiwemo wavulana 76,832 na wasichana 27,762.

Katika kipindi hicho, jumla ya operesheni 13 katika mafunzo ya JKT zimefanyika, Operesheni hizo ni pamoja na Operesheni Mkapa mwaka 2001, Miaka 40 ya JKT mwaka 2002, Utandawazi mwaka 2004 na Operesheni Jiajiri mwaka 2005.

Zingine ni pamoja na Kasi Mpya mwaka 2006, Maisha Bora mwaka 2007, Uadilifu mwaka 2008, Kilimo Kwanza mwaka 2009 na Operesheni Uzalendo mwaka (2010), Miaka 50 ya Uhuru (2011), Sensa mwaka 2012, Miaka 50 ya JKT (2013) na Miaka 50 ya Muungano (2014).

Vijana wa Kujitolea walioajiriwa
Tangu mwaka 2003 hadi 2014 jumla ya vijana 24,708 wameajiriwa katika vyombo  vya ulinzi na usalama ambapo vijana 21,977 wakiwemo wavulana 17,307 na wasichana 4,670 wameajiriwa na Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Jeshi la Polisi vijana 3,965 wavulana wakiwa 2,943 na wasichana 1,022, Magereza vijana 2,139 wavulana 2,044 na wasichana ni 95, Zimamoto vijana 100 wavulana wakiwa ni 78 na wasichana ni 22 na taasisi zingine vijana 592

Vijana 1,622 wameajiriwa katika taasisi mbalimbali kama TANAPA, GEITA GOLD MINE, BANDARI na AFRICAN GOLD MINE.

Ni vema vijana hao wakatambua kuwa tatizo la ajira sio kwao peke yao, ni tatizo la ulimwengu mzima Tanzania ikiwemo, wanashauriwa kutumia stadi za kazi kujiajiri wenyewe.

Aidha, vijana hao watambue kuwa walikula kiapo cha UTII, wakati wa kuhitimu mafunzo ya JKT, hivyo suala la kuandamana ni kinyume cha kiapo chao. Vijana hao walitumikia Jeshi la Kujenga Taifa Operesheni za nyuma na kumaliza mkataba wa miaka miwili. Shinikizo lao la kulazimisha ajira kwa kuandamana ni kinyume cha sheria za nchi.

Kwa maelezo ya hapo juu utaona kuwa Jeshi la Kujenga Taifa, halina dhamana ya kuajiri bali kufunza vijana wa taifa hili umoja, stadi za kazi na uzalendo baada ya hapo wenye sifa za kuajiriwa hupata ajira katika taasisi mbalimbali za serikari na binafsi.

Taarifa hii Imetolewa na Makao Makuu
ya Jeshi la Kujenga Taifa.



Wednesday, February 18, 2015

Yanga, Azam vitani ligi kuu Tanzania Bara


Vita ya kugombea usukani wa ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya vilabu ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kati za Azam FC na Yanga inaendelea Alhamis.
Baada ya kushinda mechi zao za CAF nyumbani,Yanga ikiwafunga BDF XI ya Botswana (2-0)
katika kombe la Shirikisho na Azam ikiwafunga El-Merreikh ya Sudan (2-0)
katika kombe la Klabu Bingwa Afrika, timu hizo sasa zinaelekea nguvu katika mechi za
ligi, ikiwa pia ni kama sehemu ya maandalizi ya mechi zao za marudiano za
ugenini.
Yanga watasafiri hadi Botswana na Azam wataenda Khartou, Sudan wakitafuta
ushindi ili kusonga mbele baada ya Juma moja lijalo. Kuelekea mechi zao za Ligi Kuu Alhamis, kila timu
ina pointi 25,Azam ikiongoza kwa tofauti ya goli moja. Yanga itacheza na Tanzania Prisons mjini
Mbeya na Azam watacheza na Ruvu Shooting mkoa wa Pwani.
Kocha wa Yanga, Hans Pluijm ametamba kushinda, huku akikabiliwa na kibarua kigumu kingine dhidi ya Mbeya
City wikiendi hii mkoani Mbeya, kwa lengo la kuongoza ligi yenye ushindani mkubwa.
Akizungumza jana, msemaji wa Azam, Jafar Iddi amesema baada ya kuwafunga Mtibwa
Sugar 5-2 majuma mawili yaliyopita, sasa ni Azam ya Ruvu Shooting katika jitihada za kukaa mbali na Yanga katika msimamo

Thursday, January 29, 2015

BINTI WA MIAKA 22 ASHINDA MILIONI 100 ZA PROMOSHENI YA JAYMILLIONS YA VODACOM

Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akifafanua jambo kuhusiana na mshindi wa shilingi Milioni 100/-kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo ambapo Mkazi wa kilolo mkoani Iringa Bi.Uwezo Magedenge aliibuka na ushindi wa kitita hicho katika droo ya 14 iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam leo,Wengine ni Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania Mrisho Millao(Kushoto) na Afisa wa kampuni hiyo Pristin Lyatonga.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.

Mkazi wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Uwezo Magendenye (22) , leo ameibuka mshindi wa kwanza wa shilingi milioni 100 katika droo ya kumi na nne ya promosheni ya Jaymilioni inayoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania.

Magedenge binti mwenye umri wa miaka 22 ambaye ni mhudumu wa mapokezi katika nyumba ya wageni ya Luganga Lodge iliyopo wilayani Kilolo amesema kuwa amepokea taarifa hizi kwa furaha akiwa kazini na amefurahia ushindi huu ambao anaamini utabadilisha maisha yake kwa kiasi kikubwa.

“Katika maisha yangu nimeishapitia mambo mengi nahangaika na maisha hadi kufikia hapa nilipo nikiwa mhudumu kwenye nyumba ya wageni.Kwa ushindi huu naamini nitafungua shughuli zangu za biashara ikiwemo kuanzisha biashara ya maduka ya M-Pesa pia kufungua nyumba yangu ya kulala wageni na kusaidia ndugu zangu ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za maisha”.Alisema.

“.Nashukuru Vodacom kwa kuleta promosheni hii ambayo naamini itabadilisha maisha yangu na namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniona na kusikiliza sala zangu .

Aliongeza kuwa kwa muda mrefu amekuwa akishiriki kwenye promosheni mbalimbali na hajawahi kufanikiwa kwa ushindi huu anaamini kuwa promosheni hizi hususani za Vodacom ni za kweli na amewataka wateja wote kushiriki ili kutopoteza bahati zao za kujishindia mamilioni ya fedha na kubadilisha maisha yao.

Akiongea muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi, Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania,Rene Meza amempongeza mshindi na kuwahimiza wateja wote kuchangamkia promosheni hii kwa kuhakikisha wametuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza nafasi zao za kushinda pia alisema kuwa njia nyingine ya kushinda ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-.

Naye Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania alisema kuwa tangu promosheni hii ianze mapema mwezi huu tayari wateja 2 wamekwishajishindia milioni 10 na wateja watano wameishajishindia shilingi milioni moja kila mmoja na maelfu wengine tayari wamejishindia muda wa maongezi.

“Promosheni hii itadumu kwa muda wa siku mia moja hivyo leo ni droo ya kumi na nne hivyo bado kuna mabilioni ya fedha yamewasubiri watanzania,wanachopaswa kufanya ni kuhakikisha kila siku wameangalia kama namba zao zimeibuka na ushindi kwenye droo ya siku kwa kutuma neno Jay kwenda namba 15544.

Thursday, January 29, 2015

BUSARA ZA MICHAEL WAKUDATA.

Friday, January 23, 2015

Ligi kuu Tanzania kuendelea Jumamosi



 
Ligi kuu ya Tanzania itaendelea Jumamosi hii huku mechi kadhaa zikichezwa ikiwemo ile kati ya bingwa mtetezi na wawakilishi wa nchi katika michuano ya klabu bingwa Afrika, Azam FC na Simba Sports Club ikiwa chini ya kocha Mserbia, Goran Kopunovic.
Azam inaongoza ligi ikiwa na pointi 20 na baada ya mechi yao na Simba itaenda Jamhuri ya Kongo (DRC) kwa ajili ya kucheza mechi za majaribio kwa ajili ya mechi yao na vigogo wa Sudan, El-Merreikh katika mechi ya kwanza klabu bingwa Afrika itakayochezwa Dar es Salaam kati kati ya mwezi ujao.
Mabingwa wa zamani wa Tanzania na wawakilishi wa nchi katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika, Yanga, ikiwa ya nne katika msimamo na alama (points) 15, watacheza na Polisi Morogoro wakati Mtibwa Sugar, ikiwa ya pili na alama 17, watacheza na Ruvu Shooting.
Mechi nyingine ni kama ifuatavyo
Stand United vs Coastal Union-Uwanja wa Kambarage,Shinyanga
Kagera Sugar vs Ndanda-Uwanja wa Kaitaba, Kagera
Mbeya City vs Tanzania Prisons-Uwanja wa Sokoine, Mbeya